Ijumaa 30 Oktoba 2026 - 00:30
Bahrain Yaendeleza Wimbi Kuwakama Wahutubu na Waombolezaji wa Kidini

Hawza/ Utawala wa Aal Khalifa, ukiendeleza vita vyake visivyo na huruma dhidi ya Waislamu wa Kishia nchini Bahrain, umewakamata wahutubiaji kadhaa wa Husseini na waombolezaji wa kidini kwa sababu ya kuandaa na kushiriki katika hafla za kuomboleza kumbukumbu ya kuuawa shahidi Bibj Fatima Zahra (sa).

Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, utawala wa Aal Khalifa umewakamata baadhi ya wahutubiaji wa Husseini na waombolezaji wa kidini kufuatia ushiriki wao katika hafla za kuomboleza kifo cha kishahidi cha Bibi Fatima Zahra (sa).

Vyombo vya usalama vya utawala wa Aal Khalifa vimemkamata mkuu wa Husseiniyah ya Haj Ahmad bin Khamis, Ustadh Habib Abbas Khamis, pamoja na mwombolezaji wa kidini Jalal al-Biladi, na kuwapeleka mbele ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka. Ofisi hiyo iliamuru waendelee kuzuiliwa kwa muda wa wiki moja ili uchunguzi uendelee. Mbali na hayo, mwombolezaji mwingine wa kidini anayeitwa Abdullah al-Matruk pia amekamatwa baada ya vikosi vya usalama kuvamia nyumba yake.

Vilevile, mhutubu wa Husseini, Mulla Habib al-Dirazi, amekamatwa kwa sababu ya kusambaza faili la sauti lenye kisomo cha Ziyara ya Ashura.

Aidha, imeripotiwa kwamba Amer Ahmad Qarqur, mkuu wa kamati ya msafara wa maombolezo katika Husseiniyah ya Jufair, pamoja na naibu wake Hussein Jaafar Mahdi, nao wamekamatwa kwa sababu ya kushiriki katika shughuli za kuratibu na kuandaa matukio ya kidini yanayohusiana na kumbukumbu ya kuuawa kishahidi Bibi Fatima Zahra (as).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha